• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

WAFUGAJI Songea waaswa kujisajiri ili watambulike kisheria

Tarehe ya Kuwekwa: September 17th, 2020


Wafugaji Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wametakiwa kujisajili na kutambulika kisheria katika maeneo wanayoishi ili serikali iweze kuwahudumia kulingana mahitaji yao.Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo Dr.Erick Kahise ametoa wito huo wakati alipokutana na kufanya kikao na wafugaji  katika cha Kijiji cha Nambendo kata ya Ndongosi.

Dr.Kahise amesema usajili wa mifugo utawezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wafugaji kufuatia takwimu sahihi zilizotolewa na wafugaji wenyewe waliopo katika eneo husika.Dr.Kahise amesema takwimu zitasaidia pia kutenga maeneo ya malisho,ujenzi wa majosho,dawa za uchanjaji wa mifugo,uwekaji wa miundo mbinu na huduma nyingine za kiutalam.

Dr. Kahise ameyataja magonjwa 13 ya kipaumbele ambayo serikali inataka wafugaji kutilia mkazo katika suala zima la chanjo  ni homa ya mapafu,mapele ya mbuzi, kideli,kimeta,kichaa ya mbwa,diganakali,bondela ufa, kutupa mimba,misona,mapele ya ngozi na magonjwa mengine ya kuku.

Amewaagiza wafugaji hao kutokiuka Sheria namba 17 ya mwaka 2003 inayosimamia mifugo kufuata taratibu za kuchanja mifugo kwa sababu chanjo inaboresha afya ya mifugo na kwamba mifugo ikiimarika na uchumi wao pia utaimarika na serikali itakusanya maduhuri,sanjari na kuimarisha lishe katika familia.“kwa mwaka chanjo itatolewa mara mbili,na bei za chanjo hizo ni bei elekezi ya serikali ambayo haizidi shilingi.1000,na adhabu ya kutochanja mifugo inafikia hadi shilingi 20,000’’,alisema.

Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Nambendo  Shaibu Rashidi Makomba amesema mpaka Septemba 15 ,2020 wamesajili wafugaji 17 kati ya wafugaji 115.Amesema idadi ndogo ya wafugaji waliojitokeza kujisajiri inasababishwa na  udanganyifu unaofanywa na wafugaji hao kuficha ukweli kuhusu idadi kamili ya mifugo wanayo miliki.Ametoa rai kwa wafugaji na wakulima katika Kijiji hicho kushirikiana katika shughuli za maendeleo  na kuacha tabia ya kuendekeza migogoro isiyokuwa na tija kwao.

Halmashauri ya wilaya ya Songea imetenga maeneo ya machungio katika kata za Muhukuru Lilahi,Muhukuru barabarani na Ndongosi.

Imeandikwa na

Jacqelen Clavery -Afisa Habari

Songea DC

 

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa