Wachungaji,mapadre,wazazi na walezi kuchukuliwa hatua za kisheria
Wachungaji,wazazi na mapadre watakao fungisha ndoa watoto wa kike chini ya miaka 18 watakuchukuliwa hatua za kisheria
Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mh Rajabu Hassan Mtiula katika sherehe za kuwaaga wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Muhukuru zilizo fanyika hivi karibuni shuleni hapo.
Mh Mtiula amesema wachungaji mapadre na wazazi watakao thubutu kuwafungisha ndoa watoto wakike wenye umri chini ya miaka 18 watachukuliwa hatua za kisheria pamoja na kuwafunga jela endapo sheria itawabaini kuwa na makosa.
Amewataka wazazi na walezi kutoa kipaumbele cha kuwasomesha watoto wakike na siyo kuwa ozesha mapema na kuwapotezea kabisa mwelekeo wa maisha yao ya baadae katika kujitafutia mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw Augustino Ndunguru amesema shule ya sekondari ya Muhukuru imefanikiwa katika ukarabati na ujenzi wa miundo mbinu ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza vizuri kama ukarabati wa maabara ambao uligharimu kiasi cha shilingi milioni kumi na ukarabati wa wa vyoo ambao ulighalim shilingi laki tano.
Mafanikio mengine ni uwepo wa umeme wa sola ambao unatoa fursa kwa wanafunzi kujisomea wakati wa usiku,ujenzi wa hostel kwa ajili ya wasichana ambao umesaidia sana kupunguza tatizo la utoro shuleni hapo.
Bw Ndunguru amesem pamoja na mafanikio hayo shule inakabikiwa na changamoto zikiwemo ukosefu wa hostel ya wavula,ukosefu wa maji,bwalo la chakula na upungufu wa vitabu vya kwa masomo hasa ya Sanaa
Jumla ya wanafunzi 13 wamefanikiwa kuhitimu kati yao wavula saba na wasichana sita huku aidadi ya wanafunzi wote ni 122.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa