Viongozi nane wa vyama vya siasa katika Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma wamepewa mafunzo elekezi ya kutambua kanuni,taratibu na sheria za mwendo na mchakato wa uchaguzi mkuu wa oktoba 28 /2020.
Mafunzo hayo yametolewa na msimamizi mkuu wa wa uchaguzi Jimbo la Peramiho Bw Simon Bulenganija katika ukumbi wa mkutano wa jimbo la Peramiho uliopo katka ofisi ya Mkurugenzi Songea hivi karibuni
Bw Bulenganija amewasihi viongozi wa vyama hivyo kusoma na kuelewa vizuri kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi kama zilivyo elekezwa na Tume ya uchaguzi Tanzania.
“Uchaguzi ni wa uhuru na haki kupitia zoezi hili lakujengeana uwezo muelewe vizuri na kutoa taarifa sahihi ili kuepusha na kupunguza malalamiko yanoweza kujitokeza katika zoezi zima la uchaguzi “,alisema Bulenganija
Amesema mafunzo hayo yanalengo la kutumiza wajibu, nao kama viongozi wa vyama vya siasa wanawajibu wa kutoa maelekezo sahihi kwa wagombea wao ,mawakala na wadau wengine wa vyama, hivyo wazingatie maelekezo yote yanayo tolewa na Tume ya Uchugazi ya Taifa kwa nia ya kuepusha sintofahamu ambazo zinaweza kutokea.
Ibrahimu komba ni katibu wa UDPP wa Wilaya ya Songea ametoa pongezi na shukrani kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo pamoja timu yake kwa kuwakuwapa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kutekeleza wajibu wao katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa kuwachagua madiwani,wabunge na Rais.
Viongozi walioshiriki mafunzo hayo ni kutoka vyama vya siasa vya ACT Wazalendo,NCCR mageuzi ,Chama cha CHADEMA,Chama cha Mapinduzi,(CCM),UDPP,Chama cha wananchi (CUF),ADATADEA pamoja na NRA.
Imeandikwa na Jacquelen Clavery
Afisa Habari-Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa