BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Songea limewataka watendaji wa kata na Vijiji kuwajibika kusimamia miradi yote kikamilifu ambayo ipo katika maeneo yao
Agizo hilo nimetolewa na Baraza la Madiwani kwenye kikao cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Lundusi-Peramiho.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menas Komba alisema wao kama baraza la madiwani wamewataka wataalamu wasimame imara katika swala zima la usimamizi wa mapato hili Halmashauri iweze kwenda mbele.
Mheshimiwa Menas alisema niwajibu wa kila kiongozi wa kata katika Halmashauri hiyo kusimamia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha katika miradi yote inayojengwa kwenye maeneo yao ili iweze kwenda vizuri na kukamilika kwa wakati.
“Lakini niwaombe waheshimiwa madiwani na viongozi wa kata mkasimamie majengo na mkayaelewe mamlaka yenu kama viongozi wa kata msikubali kuona miradi inayotekeleza na fedha za Serikali kupitia kodi za wananchi kujengwa chini ya kiwango” alisema komba.
Aidha Mheshimiwa Menas amemuagiza Mkurugenzi Ndugu Neema kwa kushirikiana na wataalamu wa Idara ya Kilimo, mifugo na uvuvi kuhakikisha wanasimamia vizuri swala la ruzuku na kuhakikisha wakulima wanapata mbegu zilizo bora kwakua msimu wa kilimo umekaribia.
Mheshimiwa Menas amempongeza Mkurugenzi Ndugu Neema na wataalamu wote wa Halmashauri kwa utendaji kazi wao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Magembe amesema maagizo yote yaliyotolewa yanalenga kuifanya Halmashauri inakwenda mbele na ili tufanye vizuri hivyo amelihakikishia Baraza hilo la madiwani kuwa maagizo yote ya kikao hicho yatafanyiwa kazi kwa ufanisi mkubwa kwa kushirikiana na viongozi wa kata
“Nipende kukuhakikishia Mheshimiwa Mwenyekiti mbele ya baraza lako kuwa haya maagizo yote ni yakwetu tuingie kazini tukafanye kazi vizuri hivyo niwasisitize watalamu turudi na majibu ya hiki tulichoelekezwa na baraza ili”, alisema Ndugu Neema.
Maagizo hayo yamekatokana baada ya kusomwa kwa taarifa ya kamati mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa