Naibu waziri wa Elimu TAMISEMI Mhe.David Silinde ametoa wito,kwa vijana kuenzi na kuthamini historia na tamaduni za kwetu kwa kufanyakazi kwa lengo la kuendeleza na kukuza uchumi wanchi kupitia utalii wa historia na utamaduni.
Mhe.Silinde ameyasema hayo wakati akifungua sherehe za kumbukizi la miaka 115 la mashujaa wa vita vya majimaji zilizofanyikika katika viwanja vya Makumbusho Manispaa ya Songea.
“Haitakuwa na maana yoyote ya kuwaenzi mashuja wetu huku tamaduni na maadili tuliyorithi toka kwa wazee wetu yakiporomoka”,amesisitiza Mhe.Silinde.
Ameongeza kwa kusema njia nyingine za kuwaenzi mashujaa hao wa vita vya majimaji ni pamoja na kupambana na rushwa,madawa ya kulevya,ujangiri,kulinda rasilimali za nchi na kuhifadhi historia za utamaduni zetu.
Kumbukizi la mashujaa wa vita vya majimaji ni kumbukizi la 115 tangu kunyongwa kwa mashujaa hao na nitamasha la 13 tangu lianzishwe.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa habari
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa