Wananchi wa Kata ya Mbinga mhalule wameanza kunufaika na huduma za afya baada ya kituo cha Afya Nakahegwa kuzinduliwa na kuanza kutoa huduma
Uzinduzi wa Kituo hicho umefanywa na (MB} wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge.Ajjira,Vijana na wenye Ulemavu Mh Jenista Mhagama hivi karibuni katika Kijij cha Nakahehegwa Kata ya Nakahaegwa Halmashauri yaSsongea Mkoani Ruvuma.
Mh Mgama amesema uzinduzi wa Kituo hicho umerahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kujitolea pale wanapotakiwa kufanya hivyo.
“ Asilimia miamoja ya wasichana wanaopima vvu, 85% wanakutwa namaabukizi na wenye umri wakuanzia miaka 15 hadi 25 baadhi ya wanaume tuache kuwafuta masichana na kufanyanao mapenzi”.Alisema Mhe.Mhagama
Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho, Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma kwaniaba ya Mganga mkuu wa Wilaya Bw Adamu ngunga amemwomba Mh Mhagama kuwasaidia kusimamia upatikanaji wa watumishia 150 wa Idara ya Afya ,gari la wagonjwa na Tsh milioni 300 kwaajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miundo mbinu ya majengo yanayohitajika.
Ujenzi wa kitauo hicho ulianza mwaka 2011 kwa wananchi kuanza kujitolea kufyatua tofari na kujenga boma,huku serikali imetoa shilingi milioni 122.5 kwa ajili ya ununuazi wa vifaa vya viwandani , ujenzi wa nyumba moja ya mtumishi na kuwalipa mafundi.
Uzinduzi wa kituo hicho cha Afya unatoa huduma kwa wananchi wa Vijiji vya Lipokela,Mbinga muhalule,Nakahegwa na Vitongoji vyake wapatao zaidi ya elfu24.
Aidha wananchi wameshukuru serikali kwakuwasogezea huduma za afya karibu jambo ambalo litawasaidia kufanya shughuli nyingine za kiuchumi kwasababu walikuwa wakitembea umbalii mrefu wakilometa 25 kutafuta huduma hiyo .
Kaimu mganga mkuu wa wilaya ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano baina yao na watumishi ili wawezekuwapatia huduma stahiki na kuacha vizingizio.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa