Uwekezaji
Halmashauri ya Wilaya ya Songea imetoa vipaumbele 10 vya maeneo ya uwekezajiji ambayo wawekezaji wanakaribishwa kuwekeza katika sekta za kiuchumi,kiutmaduni na sanaa
Vipaumbele hivyo vimetolewa baina ya wataalam wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na wadau kutoka Taasisi ya Economics and Social Research Foundation toka Dar-salaam ikiongozwa na Dr Hoseana Lunugelo katika kikao kilchofanyika katika Ofisi za Halmashauri hiyo hivi karibuni.
Maeneo yaliyo pewa vipummmbele kati ka uwekezaji pamoja na kililimo cha alizeti, kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti,kilimo cha zao la miwa,uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe,madini ya ejenzi,kuzalisha mitamba maeneo mengine ni kiwanda cha kukamua maziwa ya soya,kiwanda cha kusindika sukakari,kiwanda cha kusindika matunda na maeneo ya utalii.
Halmashauri imetoa vipaumbele kwenye maeneo hayo kwakuwa tayari maeneo yameshatengwa na uhitaji wa huduma hizo kwa jamii ni mkubwa hivyo mwekezaji atakaye kidhivigezo atapimiwa maeneo kwa mujibu wa kanuni,taratibu na sharia za nchi.
Dr Lunugelo amesema zipo faida nyingingi katika uwekezaji ambazo ni pato la mtu binafsi kutotokana na shughuli ndogo ndogo atakazozifanya katika eneo husika,na upatikanaji wa huduma za jamii kama huduma za afya,Elimu na maji na pato la serikali kwa kulipa kodi mbalimbali
Aidha wanachi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa wakezaji ambao tayari wemewekeza na wanatarajia kuwekeza katika maeneo yao kiulinzi na kiusalama.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea imeshapima maeneo ya uwekezaji katika kata ya ndongosi ekari 1000,Muhukuru Lilahi 50,000,Magwamila ekari 1000 maeneo mengine ni Nakawale ekari 1000 Nambendo ekari 50000 na Muhukuru ekari 50,000
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa