Mapato
Halmashauri ya wilaya ya songea imepanga mikakati mipya ya kukusanya mapato lengo likiwa kuvuka asilimia 50
Hayo yamesemwa na mwekahazina wa Halmashauri hiyo Bw Rajabu Lingoni katika mkutano wa Baraza maalum la kufunga mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka 2016/2017 baraza lilifanyika hivi karibuni akatika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Bw Lingoni amesema Halmashauri imepanga mikakati mipya ya kukusanya mapato na kuhakikisha inavuka lengo la kukusanya zaidi ya asilimia 50.
Ametaja baadhi ya mikakati ni pamoja na kuunda timu ambayo itasimamia ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha fedha zote zinafikishwa bank,mkakati mwingine ni vikao vya pamoja baina ya watendaji wa kata na timu ya kukusanya mapato ya Halmashauri, pia kusimamia sharia za ukusanyaji ushuru na tozo mbalimbali.
Aidha Waheshimiwa madiwani wakichangia hoja kwa nyakati tofauti wamesema ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo haukuwa tatizo,tatizo lilikuwa tofauti ya makusanyo na kiasi kinacho pelekwa bank kilikuwa hakilingani.
Kufuatia kadhia hiyo Waheshiwa madiwani wameitaka timu hiyo kufanya kazi yao kwa weledi na kutolea taarifa kwa kila robo na kuongeza kwakusema licha ya kuwepo kwa timu hiyo jukumu lakusimamia ukusanyaji wa mapato niletu sote hivyo kila mtu awajibike kweye eneo lake kazi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa