Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Mipango na Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, jana 27/05/2024 wameendelea na mkakati wao wa kuhakikisha miradi yote ya Serikali inakamilika kwa wakati na kwa usahihi, kabla ya mwaka ujao wa fedha 2024/2025.
“ Watumishi wenzangu, tunafahamu kwamba tunaelekea mwisho wa mwaka wa Fedha 2023/2024, hivyo basi bado kipaumbele chetu kiwe kukamilisha miradi yote ambayo ilishatengewa Fedha, ili kabla ya mwaka mpya wa fedha tuwe tumekabidhi kwa wananchi na waanze kupata huduma, ambalo ndilo lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Timu hiyo ya Wataalamu kutoka Halmashauri ya Songea, 27/05/2024, walitembelea na kukagua miradi ya Ujenzi katika kata tatu ambazo ni Mbingamhalule, Magagura, na Kizuka.
Wamekagua miradi mbalimbali ya Ujenzi kama vile Ghala la Matomondo ( ambapo ndipo lilipo soko la Kimkatati), Shule ya Msingi Matomondo ambapo walikagua ujenzi wa Matundu nane ( 8) ya Vyoo.
Shule ya Msingi Lusango, walikagua ujenzi wa matundu 23 ya Vyoo, Magagura Sekondari Ujenzi wa Maabara na Kizuka Sekondari wamekagua Ujenzi wa jengo la TEHAMA na Maktaba
Akizungumza kwa niaba ya timu, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Songea Bi Elizabeth Gumbo, ameendelea kusisiza matumizi sahihi ya Fedha za Serikali katika Miradi, pamoja na kuzingatia muda ili kuhakikisha kabla ya mwaka mwingine wa Fedha kuingia tuwe tumemaliza kazi zote za mwaka wa fedha 2023/2024.
Aidha Mkurugezi ametoa wito kwa wakuu wa idara na kamati za ujenzi kuhakikisha wanawakagua mafundi mala kwa mala ili kuhakikisha mafundi wanajeng kwa ubora ulikusudiwa
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa