Ujenzi wa shule
Wananchi wa kitongoji cha Ulamboni kijiji cha kizuka wanaendelea na kazi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne na ofisi mbili baada ya kukamilisha vyumba viwili ambavyo vinatumika.
Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw Abdalah Mturi ametoa ufafanuzi huo kwa kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Joel Mbewa pamoja na Uongozi wa idara ya Elimu Mkoa katika ziara ya katembelea na kukagua ujenzi wa mkondo wa shule ya Ulamboni unavyoendelea.
Bw Mturi amesema wanachi wa kitongoji cha Ulamboni Kijiji cha Kizuka kata ya Kizuka waliahamasishana kuanza ujenzi wa mkondo shule ya kwa kuanza na darasa la MEMKWA mwaka 2015 likiwa na wanafuzi 72 wakitumia banda kama darasa na mwaka 2016 walianza ujenzi wa vyumba viwili na ofisi moja ya walimu na kukamilisha kwa Jitihada za Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama, Halmashauriya Wilaya ya Songea na uongozi wa kijiji cha kizuka.
Bw Mturi amesema kwasasa wanafuzi wanasomea ndani ya vyumba vya madarasa jumla yao wanafunzi 218 wa darasa la kwanza mpaka la tano ina walimu wawili na kwakadiri ya miongozo ya Wizara ya Elimu Sayansi naTeknolojia wanakidhi mahitaji ya ufundishaji.
Amesema kwasasa wanaendele na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na ofisi mbili ambavyo vinatarajia kukamilika katika hatua ya uezekaji mwezi Novemba 2018, ujenzi huo unaenda sambamba na ujenzi wa vyoo bora vyenye matundu 8 vikiwa na mgawanyo wawavulana matundu 4 na wasichana matundu 4
Aidha Bw Mbewa amemwagiza Mkurugenzi Mtendajiwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea anapeleka vifaa vya kiwandani mapema kwaajili ya ukamilishajiwa majengo ikiwemo choo.
Mahitaji ya huduma za jamii kama vile zahanati , vituo vya afya, shule, maji na miundombinu ya barabara ya naongezeka kufuatia hali ya jamii kuhama hama makazi yao ya awali na kufuata maeneo ya kulima na kusababisha adha kwa watoto kusoma umbali mrefu.
Mkondo wa shule Ulamboni ni shule shikizi Ikiwa imegawanywa toka shule ya msingi Kizuka ambapo kabla ya madarasa kujengwa watoto walikuwa wakisoma shule ya msingi Kizuka na Mbiro umbali wa kilomita 8 kutoka kitongoji cha Ulamboni .
JACQUELEN CLAVERY -TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa