UJENZI NA UKARABATI WA MIRADI YA MAJI
Halmashauri ya wilaya ya Songea imefungua zabuni ya ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu ya miradi ya maji katika kijiji cha Matimira na Mbiro
Zabuni hiyo hiyo imefunguliwa hivi karibuni na kaimu Afisa manunuzi wa H/mashashauri Bw Andrew Nzali katika kikao cha pamoja baina ya waomba zabuni na wajumbe wakikao hicho kilicho fanyika septemba 18 /2018 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Akifungua zabuni hizo amesema zabuni zilizoombwa ni mbili na makampuni yalijitokeza kuomba kufanya kazi ya ujenzi na ukarabati wa miradi hiyo ni nne ambazo ni ARM COMMONICATION COMPANY LTD kutoka Mkoa wa Njombe, NGOGO COMPANY LTD kutoka njombe,STUIMAK COMPANY LTD na SHADA INVESTMENT COMPANY zote kutoka Manispa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Amesema ujenzi wa mradi wa maji Mbiro umeombwa na kampuni ya SHADA INVESTMENT COMPANY ambapo wameomba kujenga mradi huo kwa muda wa miezi mitano,na kampuni ya ARM COMMONICATION COMPANY wao wameomba kujenga mradi huo kwa muda wa miezi mitano pia.
Bw Nzali amesema mradi wa ukarabati wa miundo mbinu ya maji katika kijiji cha Matimira umeombwa kukarabatiwa na kampuni ya STUIMAK COMPANY LTD wameomba kukarabati kwa kwa muda wa miezi mitano na NGOGO COMPANY LTD wameomba kukarabati kwa muda wa miezi mitano pia.
Aidha Bw Nzali amesema mchakato wa kumpata mkandarasi wa kila mradi unaendelea kupitia vikao husika pindi zoezi litakapo kamilika na utekelezaji wa kazi hizo utaanza.
Ukarabati wa miundo mbinu ya maji unaotarajia kufanyika katika kijiji cha Matimira ni kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji kwa wananchi kwakujenga mtandao wa usambazaji wa maji na ujenzi wa tank jipya lenye ukubwa wa Zaidi ya lita 250,na ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mbiro ni kuondoa changamoto ya maji kwa wananchi wa kijiji hicho ambao kwasasa wanatumia maji mtiririko yanayo patikana kwa wingi kidogo .Wananchi wanatakiwa kutunza vyanzo vya maji kwa ustawi wa maisha ya wanyama na mimea.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa