Ufunguaji wa miundo mbinu
Halmashauri ya wilaya ya Songea kwa kushirikiana na kampuni ya Global Grid LTD wamefungua miunndo mbinu ya barabara katika kijiji cha Lundusi kilichopo mji mdogo wa Peramiho.
Meneja wa kampuni hiyo Bw Alfred Manjoro amasema hayo katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari akiwa eneo la kazi hivi karibuni.
Bw Manjoro amesema walianza na hatua ya kwanza ya kupanga maeneo kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi,hatua ya pili walifanya upimaji wa viwanja na kuweka alama mbalimbali na hatua ya mwisho ni ya kufungua miundo mbinu ya barabara.
AMESEma upimaji huu umehusisha wananchi wa kijiji cha Lundusi,aHalmashauri na Kampuni kwa makubaliano kwamba wananchi watapata asilimia 60 ya viwanja na kampuni itabaki na asilimia 40 ambayo ni gharama za kuwapimia viwanja wanachi,upimaji wa maeneo na ufunguaji wa miundo mbinu nakulipia kodi.
Ameongeza kwa kusema kwa kuanzia wamepima viwanja 3500 katika vitongoji vya Dodoma,Chemchem,Lundusi,Mtakuja na vingine ni Linga na Mandela.
Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw Mendradiusi Aliyafao amesema mpango huu ni mkakati wa kurasimisha Mji mdogo wa Peramiho ili wananchi waweze kumiki maeneo yao kisheria pia ametoa rai kwa vijiji vingine kuiga mfano wa kijiji cha Lundusi kwa kupimiwa maeneo waweze kuyamiliki kisheria na Kampuni ipo tayari kuwapa huduma hizo.
Jacquelen clavery -tehama
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa