Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Peramiho, Ndugu Ignus Kong’owa, amesema maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 yanaendelea vizuri huku kampeni zikiendelea kwa amani katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Akizungumza leo Septemba 12, 2025 ofisini kwake na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Kong’owa alisema kuwa hadi sasa kampeni zimeingia siku ya 16 kati ya siku 62 zilizopangwa kwa ajili ya kampeni za kisiasa.

Alibainisha kuwa vyama vitatu vya siasa ambavyo ni CHAUMA, ACT-Wazalendo na CCM tayari vimeshazindua kampeni zao na zinaendelea katika kata mbalimbali za Jimbo la Peramiho.
“Mpaka sasa hakuna changamoto yoyote kubwa iliyojitokeza, Tunaendelea kufuatilia mwenendo wa kampeni ili kuhakikisha zinafanyika kwa utulivu na amani, sambamba na matumizi ya lugha za staha,” alisema Kong’owa.
Aidha, aliwaasa wanasiasa na wafuasi wao kuendelea kudumisha amani na mshikamano wakati wote wa kampeni, akisisitiza umuhimu wa kutumia lugha nzuri isiyo na mivutano.
Kauli mbiu ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 inasema “Kura yako haki yako, jitokeze kupitia kura” kauli mbiu hii inamaana kwamba kila raia mwenye sifa ya kupiga kura ana haki ya kikatiba ya kuchagua viongozi anaowaona wanafaa, na njia pekee ya kuitumia haki hiyo ni kwa kushiriki kupiga kura.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa