Ubalozi wa kabidhi magari.
Ubalozi wa watu wa Marekani Nchini Tanzania umekabidhi magari sita aina ya Toyota Hilux kwa waratibu wa Mikoa Mitano wa mradi wa Mwitikio wa Kudhibiti UKIMWI Mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Magari hayo yamekabidhiwa na kaimu Balozi wa Serikali ya watu wa marekani Nchini Mhe.Inmi Patterson katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya bustani ya Manispa ya Songea hivi karibuni.
Mhe Patterson amesema Serikali ya Watu wa Marekani inataka kuona Watanzania wenye maambukizi ya VVU na wenye ukimwi wanaishi maisha yenye ustawi na afya njema na wanaendelea kufanya kazi na kuchangia na kukuza uchumi wa Nchi.
Amesema kwa muda mrefu waratibu wameshindwa kutekeleza na kusimamia shughuli za uratibu na uwajibikaji Kitaifa kutokana na ukosefu wa rasilimali hivyo kupitia rasilimali hiyo wakatekeleze majukumu yao.
Akipokea magari hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Mhe Jenista Mhagama amemewataka waratibu waliokabidhiwa magari wahakikishe yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na atafutilia kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS na kuchukua hatua kali dhidi yao
Amesema agenda ya mapambano dhidi ya UKIMWI ni moja ya agenda za serikali ya awamu ya tano,hivyo kila Mkoa uwenamipango yake ya namna ya kudhibiti UKIMWI nabaadae iwezekujadadiliwa kikanda na kufanyiwa maamuzi.
Mikoa iliyokabidhiwa magari hayo ni Ruvuma,Katavi,Mbeya,Songwe na Rukwa.
Watanzania zaidi ya milioni moja wanapata tiba ya UKIMWI,aidha maambukizi ya UKIMWI kitaifa asilimia 5.6 kutoka asilimia 7 na lengo la Serikali mungu akijalia hadi kufikia mwaka 2030 maambukizi dhidi ya VVU kuwa asilimia 0
Jacquelen Clavery
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa