Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea,Bi Elizabeth Mathias Gumbo, akiambatana na baadhi ya Wataalam wamejiandikisha kwenye Daftari la kupiga kura katika Kata ya Peramiho, Kijiji cha Lundusi kitongoji cha Dodoma
Bi. Elizabeth ametoa wito kwa wananchi wa Jimbo la Peramiho ambao bado hawajajiandikisha kuendelea kujiandikisha kwa siku zilizobaki ili waweze kuingia kwenye orodha ya watakaochagua viongozi kwenye uchaguzi utakaofanyika tarehe 27/11/2024
Judith Alex Kapinga, ni mwandikishaji katika kituo cha Dodoma, kilichopo kijiji cha Lundusi kata Peramiho baada ya ujio wa Timu ya Wataalam wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji amesema “Binafsi nimefurahi sana kiongozi kuja kujiandikisha, amekua mstari wa Mbele na baada yay eye kuja kujiandikisha kumekua na witikio mkubwa, watu wamehamasika na hata tumefika asilimia 72 mpaka sasa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa