Ukaguzi wa miradi yenye thamani ya bilioni 2.3 uliofanywa kwa ushirikiano na timu ya wataalam, ikiongozwa na mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Elizabeth Gumbo imekamilisha ziara yake jana Septemba 30, 2025 na kufanya tathmini ya kina ya miradi 59 iliyopo katika kata 16 zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ikilenga kubaini maendeleo, changamoto, na nafasi za kuboresha.

Ziara hiyo ya siku sita, ilijumuisha Wataalam mbalimbali ambao wanahusika kwa namna moja ama nyingine na Miradi inayotekelezwa kama vile Idara yenye miradi husika, Manunuzi, Mkandarasi, Muweka hazina Maendeleo ya Jamii, Mipango, Watendaji wa Kata husika, ambapo kwa uwepo wao imekua rahisi kutatua changamoto zilizokua zikijitokeza
Miradi iliyotembelewa katika ukaguzi huo ni pamoja na Ukamishaji na Ujenzi wa Madarasa, Matundu ya Vyoo, Zahanati, Vituo vya Afya Nyumba za Watumishi pamoja na Mabweni ambapo Wataalam walikagua nyaraka, walifanya mahojiano na wanajamii, na walitembelea maeneo husika ili kupata picha halisi ya utekelezaji wa miradi.
Miongoni mwa mambo yaliyogundulika ni umuhimu wa ushirikiano kati ya jamii na viongozi wa halmashauri katika kusimamia miradi hiyo. Wataalam walibaini kuwa baadhi ya miradi ilikabiliwa na changamoto za ukosefu wa rasilimali na kuhakikisha rasilimali hizo zinafika kwenye miradi kwa haraka. Hata hivyo, miradi mingine ilionyesha mafanikio makubwa katika kuboresha maisha ya wananchi, hasa katika sekta za elimu na afya.

Matokeo ya ukaguzi huu yatatumika kama msingi wa kuboresha usimamizi wa miradi katika halmashauri, kuhakikisha kuwa rasilimali zinatumika ipasavyo na miradi inatoa matokeo chanya kwa jamii. Mkurugenzi alisisitiza umuhimu wa kuendelea na ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha uwajibikaji na ufanisi katika utekelezaji wa miradi yote
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa