Watoa huduma za chakula wa Halimshauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wametakiwa kuzingatia mahitaji ya kisheria katika udhibiti wa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko.
Rai hiyo imetolewa na mkaguzi wa chakula kutoka mamlaka ya chakula na dawa kanda ya Kusini Bw. Kasela Kasubi katika mafunzo ya kuwajengea uelewa watoa huduma ya chakula yaliyo fanyika katika ukumbi wa Wilaya ya Songea hivi karibuni.
Bw. Kasubi amesema watoa huduma ya chakula wanatakiwa kuzingatia mahitaji ya kisheria katika utoaji wa huduma hiyo ikiwemo udhibiti wa huduma ya chakula kwenye mikusanyiko, kukidhi vigezo vya kusajiliwa na kupata kibali cha kufanya biashara sambamba na kuzingatia kanuni za afya kabla ya kuanza biashara.
Amewataka watoa huduma za chakula kupima afya zao kitendo kitakacho saidia kuzuia magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa kama vile TB, Kikohozi, Mfua, yasiweze kuambukiza watu wengine, kupima afya ni muhimu sana kwa watoa huduma ya chakula kwa sababu kunasaidia kuwatambua walioathirika na maradhi kuazishiwa tiba mara moja.
Amesema wameamua kutoa Elimu hiyo baada ya kubaini changamoto zinazowakabili watoa huduma za chakula kwa kushindwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria kwa kujua au kutokujua na kutoa huduma kiholela jambo linaloweza kusababisha madhara ya kiafya kwa mtumiaji yakiwemo magonjwa ya milipuko.
Bw. Kasubi amesema kushindwa kutekeleza matakwa ya kisheria na kutokuzingatia kanuni za Afya adhabu yake ni kufungiwa biashara, kunyang’anywa kibali na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
``Zipo sheria zinazosimamia utoaji wa huduma za chakula kwenye mikusanyiko, shareia ya chakula, dawa na vipodozi sheria namba 219, inaweka sharti la kusajili jengo linalotumika kwa ajili bidhaa zinazo dhibitiwa na TFDA chakula ni moja ya bidhaa hizo” Alisema Kasubi.
Clementina Komba ni moja kati ya watoa huduma za chakula akizungumza kwa niaba ya wenzake katika maadhimia ya pamoja baina yao na Mamlaka ya chakula na Dawa Nchini wameomba wapewe siku tisini ili waweze kutekeleza matakwa ya kisheria katika utoaji wa huduma ya chakula kwa jamii husika.
JACQUELEN CLAVERY- TEHAMA.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa