• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

TASAF kuzifikia kaya milioni 1.45 kipindi cha pili awamu ya tatu

Tarehe ya Kuwekwa: April 20th, 2021

Mfuko wa kunusuru kaya masikini Nchini (TASAF) imepanga kuzifikia kaya masikini milioni 1.45 sawa naongezeko la kaya laki tatu kwa kipndi cha pili awamu ya tatu.

Hayo ameyasema Gerson Mboramallamia kwaniaba ya Mkurugenzi wa TASAF Nchini kwenye kikao cha kuwajengea uwezo viongozi,watendaji na wawezeshaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini kipindi cha pili awamu ya tatu kilicho fanyika katika ukumbi wa SACCOS ya Walimu Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Mboramallamia amesema azma ya Serikali kupitia  TASAF ni kupunguza umasikini wa kipato na kuongeza kipato kwenye kaya masikini kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa kuboresha huduma za jamii kama vile huduma ya maji , afya, barabara na vivuko kwa walengwa kufanyakazi.

Amesema katika awamu ya kwanza ya utekelezaji TASAF imefanikiwa kupunguza umasikini wa kaya kwa asilimia 10 na umasikini uliokithiri kwa asilimia 12 kwa walengwa kufanya shughuli za kiuchumi za ufugaji,kilimo,uvuvi,biashara ndogondogo na ajira za muda mfupi.

Ameongeza kwa kusema TASAF kipindi cha awamu ya kwanza kiliwafikia walengwa kwa asilimia 70 na kipindi hiki cha pili awamu ya tatu kimepanga kukamilisha asilimia 30 iliyobaki na kufikisha asilimia miamoja ya walengwa wote Nchini iliwaweze kunufaika na mfuko huo kupitia ruzuku za aina nne ambazo mfuko umebanisha katika kukabiliana na tatizo la umasikini

Mboramallamia amezitaja aina za ruzuku zitakazo tolewa kuwa ni ruzuku ya msingi inayotolewa kwenye kaya iliyopo kwenye mpango,ruzuku ya kutimiza masharti inayotolewa kwa kaya yenye walengwa wanaotakiwa kutimiza  masharti ya elimu na afya ,ruzuku ya walemavu inayotolewa kwa walemavu na ruzuku ya Watoto inayotolewa kwa Watoto wanaoishi kwenye kaya masikini.  

Kwaupande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Pendo Daniel ameomba TASAF makao mkuu kuwarejesha kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini walengwa ambao waliondolewa kwenye mpango baada ya kufanyika kwa uhakiki wakuzitambua kaya zinazostahili kuwepo kwenye mpango.


“Nimefurahishwa sana na maboresho ya kipindi hiki cha pili awamu ya tatu kwakufanya uhakiki na kuwabaini walengwa hewa ambao hawakustahili kuwepo kwenye mpango”,amesema Mhe.Menas Komba

Mhe. Komba amesema TASAF licha ya kunusuru kaya masikini imesaidia sana kaya hizo kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ambayo inamwezesha mlengwa na wategemezi wake watano kupata huduma za matibabu kwa gharama ya shilingi elfu 30,000 kwakipindi cha mwaka mmoja.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Simoni Bulenganija amewataka watendaji ambao wameteuliwa kufanya zoezi la uhakiki awamu hii kwenda kufanya kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa na kuzingatia kiapo walichoapa.

Bulenganija amesema katika eneo la usimamizi na ufuatiliaji amejipanga vema katika zoezi hilo ili kuhakikisha kazi ya kuibua kaya masikini zenyesifa linafanikiwa kama Serikali inavyokusudia kufanikisha mpango wake wa kunusuru kaya masikini na umasikini uliokithiri nchini.

Mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea  Hosana Ngunge amesema katika zoezi la utambuzi wa kaya masikini jumla ya wataalam tisa wameteuliwa kutekeleza kazi hiyo  katika Vijiji 24 ambavyo awali havikuwaepo katika mpango.

Halmashauri ya wilaya ya Songea inajumla ya kaya 2743,Vijiji 56 ambavyo vyote vinaingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini wa kipindi cha pili awamu ya tatu.

Mpango wa TASAF kipindi cha pili awamu ya tatu kilizinduliwa na hayati Rais Dkt John Pombe Magufuli mwaka 2020 na mpango huo utakamilika mwaka 2023.

Imeandaliwa na kuandikwa na

Jacquelen Clavery

Afisa Habari Songeadc.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa