• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

TARURA waanza ujenzi wa daraja la mto Njoka

Tarehe ya Kuwekwa: July 14th, 2023

Serikali yatoa millioni 699 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Njoka lenye ukubwa wa mita 20 na ambalo litapitika muda wote na kusaidia kufungua barabara Muhukuru mpaka Kizuka itakayochochea uchumi kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katka Halmashauri ya wilaya ya Songea leo tarehe 13/07/2023.

“Barabara hii ni barabara muhimu, ni barabara ya huduma ni barabara ya uchumi ni barabara itakayoimarisha ulinzi,” na kipekee ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja alisema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama alifafanua, serikali imetenga fedha kwa ajili ya kujenga daraja la mto Mgugusi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili madaraja yote makubwa yaweze kupitika katika majira yote ya mwaka wakati wa mvua na wakati wa kiangazi.

Aidha ujenzi wa madaraja madogo madogo manne umekamilika na wakala wa barabara vijijini TARURA wanamalizia ujenzi wa madaraja mengine manne madogo madogo yaliyobakia katika ujenzi wa barabara.

“Ukamilishwaji wa ujenzi wa barabara utarahisishia wananchi kupata huduma ya usafiri kwa haraka na kuchochea ukuaji wa Miji,” alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mhe. Menas Komba amesema ujenzi wa daraja hilo utasaidia serikali kuongeza mapato katika mazao ya bishara na chakula.

“Barabara inaenda kuwakomboa wakulima wa wilaya ya Songea kwa kurahisisha huduma ya usafiri, na tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Chama cha Mapinduzi kwa kusimamia vizuri ilani”

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Songea Vijijini Ndg. Thomas Masolwa amempongeza Mhe. Rais kwa kutatua changamoto kwa wananchi, na kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mto Njoka.

Awali katika taarifa wakala wa barabara vijijini TARURA Mhandisi Johnson Kweka alisema Mkandarasi HERA Construction ameshatekeleza kazi za kusafisha eneo la daraja, kuondoa miti katika eneo la mradi, kuchimba udongo na kupasua mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa daraja.

Amefafanua kwamba Mkandarasi anaendelea na ufungaji wa nondo na boksi kwa ajili ya ufungaji wa nguzo na mikono ya daraja na ujenzi umefika 40%



Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa