• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

TARURA Songea kutumia milioni 789 matengenezo ya barabara

Tarehe ya Kuwekwa: March 24th, 2021

WAKALA wa Barabara mijini na vijijini(TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma imeidhinishiwa shilingi milioni 789 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Meneja wa TARURA  katika Halmashauri hiyo Mhandisi John Ambrosi amesema Halmashauri hiyo ina mtandao wa barabara zenye urefu wa kilometa 1057 kati ya hizo,barabara za lami ni kilometa 13.77,kilometa 250 ni barabara za changarawe na barabara za udongo ni zaidi ya  kilometa 700.

“Katika mwaka wa fedha 2020/2021 TARURA tunatekeleza mikataba sita ya ujenzi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.396,kati ya hizo  shilingi milioni 701 ni kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Muhukuru na fedha inayobakia ni kwa ajili ya matengenezo ya barabara’’,alisema.

Hata hivyo amesema katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 TARURA ilikuwa na mradi wa ujenzi wa daraja la Muhukuru ambao unatekelezwa katika mwaka wa fedha 2020/2021.

arabara’’,alisema.

Amesema utekeleza wa miradi hiyo ulianza Agosti 2020 na kwamba hadi kufikia Novemba 2020 jumla ya miradi minne kati ya sita ilikuwa imetekelezwa ambapo hadi kufikia Juni mwaka huu miradi yote inatarajiwa kukamilika kwa asilimia 100.

Hata hivyo amesema licha ya jitihada zinazofanywa na TARURA kuimarisha barabara,madaraja na vivuko,kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazoathiri miundombinu zikiwemo magari yenye uzito mkubwa na mvua za masika zinazoanza Novemba hadi Aprili kila mwaka.

Baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Kijiji cha Litowa  wanaishukuru  TARURA kwa kuwasaidia kukarabati kivuko  kinachounganisha kitongoji cha Goliama na Litowa .

Hata hivyo Christina Njovu na Egno Mwalongo wamesema kivuko hicho  kimekuwa kero kwao  kwa sababu magari hayawezi kuvuka pia kinahatarisha usalama wao hivyo wanaiomba serikali kuwajengea daraja la kudumu.

Akizungumzia kero ya vivuko hivyo ,Meneja wa TARURA  Mhandisi Ambrosi amesema  wanatambua changamoto hiyo ambapo hivi sasa bado hawajapata fedha ya kujenga daraja la kudumu.

Amesema  TARURA imejenga kivuko cha mbao chenye urefu wa kilometa 21,na kwamba wamekuwa wanakifanyia matengenezo ya mara kwa mara wakati serikali inatafuta fedha za kujenga daraja la kudumu ili kumaliza kero hiyo kwa wananchi.

Imeandikwa na Jacquelen Clavery

Afisa Habari Songea DC

Machi 24,2021

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa