MWENGE WA UHURU 2018.
Mwenge wa uhuru umemaliza mbio zake salama katika Mkoa wa Ruvuma huku ukiacha changamoto katika miradi ya maendeleo ambayo watendaji wa serikali wametakiwa kuikamilisha.
Hayo yamesemwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw FRANCIS KABEHO wakati wa kukubidhi mwenge wa uhuru mkoani Mtwara.
Bw Kabeho amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh Christina Mndeme kpitia miradi yote ambayo imeoneka kuwa na dosari kuhakikisha inakamilika na kuwachukua hatua watendaji walioshiriki kuhujumu miradi ya serikali ambayo mwenge wa uhuru umeipitia.
Amewakata wahandisi kufanyakazi kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwakuwa zama zimebadilika hivyo kila mtu katika eneo lake la kazi afanye kazi kulingana na taratibu zilizo wekwa.
Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na Zaidi ya miradi 70 ya maendeleo,miradi 9 kati ya hiyo haikufunguliwa,kuwekewa mawe ya msingi na kuzinduliwa na mwenge wa uhuru kufuati miradi hiyo kukutwa na dosari katika utekelezajiwake.
Imeandaliwa na:
Jacquelen Clavery. TEHEMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa