Ruvuma imewataka Wananchi kutoa ushirikiano katika kudhibiti vitendo vya rushwa katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 2020.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda waTAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Bw Owen Ajasson wakati akitoa taarifa ya Utendaji kazi wa TAKUKURU kwa kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2020 katika ofisi za TAKUKURU leo.
Ajasson amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kutoa Ushirikiano wa kudhibiti vitendo vya rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa vitakavyo fanywa na wagombea mbalimbali kwa nafasi za Udiwani na Ubunge pamoja na wapambe wao.
“TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma tumejipanga kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya wagombea na kampeni zao na wapambe wao ili kuzuwia na kupambana na Rushwa” Alisema Ajasson.
Amesema Katika kipindi cha miezi mitatu Taasisi hiyo imefanikiwa kukokoa kiasi cha fedha zaidi ya Sh. Milioni 359 kutoka vyama vya Ushirika (SACCOS), kwa Wilaya ya Songea, Mbinga, na Namtumbo, Makusanyo ya Vitambulisho ya wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) kwa Wilaya ya Tunduru, Mbinga, na Halmashauri ya Wilaya ya Songea katika kijiji cha Makwaya kata ya Muhukuru- Lilahi, na maeneo mengine ni Sekta ya Elimu, Benki ya Wananchi Mbinga, na Ubadhilifu wa Makusanyo yatokanayo na POS pamoja na dhuluma dhidi ya wakulima wa zao la korosho.
Ameongeza kwa kusema katika kipindi tajwa Taasisi hiyo imefanya ufuatiliaji wa miradi 8 ya maendeleo ambayo ni ujenzi wa Miundombinu na afya yenye zaidi ya thamani ya sh. bilioni moja na milioni mia nane miradi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea na maeneo mengine ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya Magagura na Matimira na matengenezo ya Barabara ya Maposeni hadi Likingo unaosimamiwa na TARURA.
Ajasson amesema Katika ukaguzi wa Mradi wa matengenezo ya Barabara ya Maposeni hadi Likingo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ilibainika kwamba alama za Barabarani katika barabara hiyo hazijawekwa na kipande cha kiliometa 3 ambacho kilitakiwa kiwekewe kifusi hakijawekewa.
TAKUKURU kwa kipindi cha Julai- Septemba imejipanga kuendelea kuelimisha wananchi kupiga vita vitendo vya rushwa katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi oktoba 2020 ili wasikubali kurubuniwa kwa vitendo vya Rushwa na kutambua haki na wajibu wao wa kufahamu Uchaguzi ninini, lengo la Uchaguzi, sheria inayoongoza uchaguzi pamoja na umuhimu wa kupiga kura.
IMEANDIKWA NA;
JACQUELEN CLAVERY
16.07.2020
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa