Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 123,930,000 kutoka Serikali kuu Kwaajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa shamba darasa la Viumbe maji lilipopo Katika Kata ya Mpitimbi.
Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menas Komba na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Neema Maghembe katika kikao cha kamati ya fedha.
Lengo la mradi huu ni kuendeleza sekta ya uvuvi Kwa utoa mafunzo Kwa wafugaji wa Viumbe maji ili Elimu hivyo iweze kuendelezwa Kwa wafugaji wengine ndani ya Halmashauri.
Aidha, fedha hizo zinatarajiwa kujenga mabwawa ya Samaki manne, uzio na darasa la mafunzo.
Pia wamesema Halmashauri imepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 278,300,901.28 kutoka Serikali kuu Kwaajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za Msingi 8.
Shule ambazo zimepokea fedha hizo ni lihuhu, Mhimbasi, Lung'oo, Makambi, Lunyele, Jenista, Ligunga pamoja na Parangu
Aidha, Halmashauri imetoa maelekezo ya awali Kwa Watendaji wa Vijiji husika kuunda kamati za ujenzi, kuandaa tofali na kuchimba mashimo Kwa kuwa fedha hizo ni Kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya viwandani ili kukamilisha mradi kwa kuzingatia viwango vya ubora unaotakiwa katika utekelezaji wa mradi wa SWASH.
Vilevile Halmashauri kupitia Idara ya Elimu Msingi imepokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 22 Kwaajili ya ukarabati wa klasta ya walimu iliyopo katika Kata ya Mpitimbi.
Aidha, fedha hizo zimetolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na technolojia kupitia mradi wa kuimarisha mradi wa kusoma, kuandika na kuhesabu Kwa Elimu ya Msingi awamu ya pili.
Uongozi wa Halmashauri unatoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kuleta fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa