• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

SONGEA yatoa mshindi ufugaji bora samaki Nyanda za Juu Kusini

Tarehe ya Kuwekwa: August 25th, 2020

Halmashauri ya wilaya ya songea mkoani Ruvuma imefanikiwa kutoa mshindi wa kwanza kimkoa na mshindi wa pili katika Kanda ya Nyanda za Juu katika ufugaji wa samaki.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa mshindi na Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Tulia Aksoni katika maonesho ya nane nane yaliyo fanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya  hivi karibuni.

Afisa Mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya songea Dkt Erick Kahise amemtaja aliyeshinda tuzo hiyo kuwa ni Aureliusi Njerekela kutoka kijiji cha Peramiho nje kidogo ya mji wa Songea.

Dkt Kahise amesema mfugaji huyo ameshinda tuzo hiyo baada ya kushindanishwa na wafugaji ndani ya Mkoa  na Mikoa ya Nyanda za juu kusini  na kuibuka kinara katika ufugaji wa samaki.

”Ufugaji wa samaki ni fursa inanyomwinua kiuchumi mwananchi hivyo wananchi wanatakiwa kufanya ufugaji wa samaki ili kujikwamua kiuchumi”,alisema Dkt Kahise.

Kwa upande wake Bw Njelekela amesema yeye binafsi ana mapenzi makubwa ya ufugaji wa samaki na alianza kufuga samaki mwaka 2016  amendelea kufuga hadi sasa akiwa na  mabwawa sita.

Amesema kupitia elimu ya ufugaji ambayo ameipata kutoka kwa wataalamu imemsaidia kuendelea kufuga kwa kisasa kwa kutumia mabwawa ya maturubai njia ambayo inatoa mazao mazuri ya samaki ukilinganisha na mabwawa ya matope ambayo wakati wa kuvua,samaki hukimbilia kwenye mapango hivyo husababisha hasara kwa wafugaji.

Dr.Kahise amesema Halmashauri ya Wilaya ya Songea haina changamoto za magonjwa ukilinganisha na mikoa mingine na kwamba maeneo mengi yana maji ya kutosha katika kipindi kizima cha mwaka hivyo kusababisha ufugaji wa samaki kuwa ni fursa kwa mtu yeyote anayependa kufuga.

Ametoa wito kwa wafugaji wa samaki kuanza kufuga kwa kuchimba mabwawa nchi kavu ,mabwawa ambayo hayana karaha katika utunzaji wa samaki.

Ametoa rai kwa wafugaji kuanza kufuga kambale ambao wanaoneka kuwa na bei ya wastani wa shilingi ya 8000 kwa kilo moja ambapo kambale mmoja anaweza kuwa na zaidi ya kilo tatu ukilinganisha na pelage wenye kilo ndogo.

Halmashauri ya wilaya ya songea inatarajia kuanzisha kituo cha uzalishaji wa vifaranga vya samaki katika eneo la Lundusi ambapo kila mwananchi atapata fursa ya kujifunza na kununua vifaranga vya samaki.

Imeandikwa na

Jacquelen Clavery

Afisa habari –Songea DC.

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KULA YAMEANZA SONGEA DC

    April 29, 2025
  • MHE . JENISTA MHAGAMA AZINDUA MADARASA 27 NA VYOO MATUNDU 44, SONGEA DC

    March 16, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa