MKUU wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Kamando Mgema amefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa 10 Songea vijijini.
Akizungumza katika ziara hiyo amewapongeza timu ya wataalamu, baraza la Madiwani, Viongozi wa chama na kamati za ujenzi kwa usimamizi mzuri na kwa kukamilisha kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.
Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Songea ilipokea kiasi cha shilingi milioni 200 kwaajili ya ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa kwaajili ya kupokea kidato cha Kwanza mwakani.
'’ Nichukue fursa hii kuishukuru serikali yetu ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha ambazo zimetuwezesha kutatua changamoto za upungufu wa vyumba vya madarasa kwa vijana ambao watajiunga na kidato cha Kwanza mwakani”, amesema Mhe. Mgema.
Mheshimiwa Mgema ameongeza kuwa fedha ambazo Halmashauri imepokea zimefanya kazi ambayo imekusudiwa hivyo Halmashauri ipo tayari kwaajili ya kutekeleza miradi mingine ambayo italetwa.
“Sisi mara zote hatujawahi kushindwa tunapewa fedha kwa kushirikiana tunazisimamia na tunatoa matokeo yaliyokusudiwa hivyo katika eneo hili la madarasa ni ushuhuda kazi tunaiweza”, amesisitiza Mhe. Mgema.
Mheshimiwa Mgema ametangaza rasmi kazi ya ujenzi wa madarasa 10 ya kisasa imekamilika kwa asilimia 100 na tayari kwa kupokea wanafunzi wa kidato cha Kwanza mwakani.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa