HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea imefanya ziara ya ukaguzi wa Milango katika karakana ya Mpingi Mahenge ambayo itatumika kukamilisha ujenzi katika hospitali ya Wilaya Mpitimbi.
Ukaguzi huo umeongozwa na Kamanda Mkuu wa Madawati kutoka Takukuru Ndugu Saimoni Obunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe, timu ya wataalamu na wawakilishi wa kamati ya manunuzi kutoka hospitali ya Wilaya ya Mpitimbi.
Aidha jumla ya milango iliyokaguliwa ni 97 imetengenezwa kwa mbao ngumu za miti pori kama mkongo, miwawa na mininga.
Vilevile milango yote ipo vizuri na inaendelea na matengenezo ya mwisho(finishing) tayari wa kufungwa katika majengo hayo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa