Mafunzo ya maboresho ya mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa za Fedha kwa Vituo vya Kutolea Huduma (FFARS) yamefanyika katika ukumbi wa Jenista Mhagama uliopo Shule ya Sekondari Maposeni, yakihusisha wahasibu kutoka vituo mbalimbali vya kutolea huduma ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Ndugu Onesmo Kabuga, ambaye aliwataka washiriki kuyapokea kwa moyo wa uwajibikaji maboresho hayo ya mfumo. Alisisitiza kuwa maboresho hayo yanalenga kuboresha mfumo wa manunuzi na usimamizi wa fedha katika vituo vya kutolea huduma, hatua itakayosaidia kuongeza uwazi na ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Ndugu Kabuga alieleza kuwa mfumo huo utasaidia kupunguza matumizi makubwa ya karatasi, kuokoa muda pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji. “Kupitia maboresho haya, shughuli nyingi za kifedha zitafanyika moja kwa moja kwenye mfumo, jambo litakalorahisisha upatikanaji wa taarifa na kuimarisha ufanisi katika utendaji kazi wetu,” alisema.
Mafunzo hayo pia yalihudhuriwa na wakufunzi wa maudhui ya mfumo huo, akiwemo Ndugu Lameck Mkongogo, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ambaye aliwafundisha washiriki namna ya kutumia maboresho hayo kwa vitendo. Alisisitiza kuwa mfumo huo utarahisisha ufuatiliaji wa fedha katika kila kituo na hivyo kuongeza uwajibikaji. Washiriki wa mafunzo hayo walitoka shule za msingi na sekondari, hospitali, vituo vya afya, zahanati pamoja na vijiji,
Washiriki wa mafunzo hayo walionesha mwitikio chanya kwa maboresho ya mfumo wa FFARS, wakieleza kuwa utarahisisha utunzaji wa kumbukumbu na utoaji wa taarifa sahihi kwa wakati. Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuhakikisha kuwa mifumo ya kidijitali inatumika ipasavyo katika kusimamia fedha za umma ili kuchochea maendeleo endelevu kwa wananchi.
Songea DC yaendesha mafunzo ya maboresho ya mfumo wa FFARS kwa vituo vya kutolea huduma

Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa