VIONGOZI wa Chama kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Menasi Komba na Timu ya wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Neema Maghembe wameendelea na ziara ya mafunzo Mkoani Geita Septemba 20, 2022.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhe.Menasi ametoa shukrani za dhati kwa Viongozi wa Chama na Timu ya Wataalamu wa Halmashauri ya Mji Geita kwa mapokezi mazuri na kujitoa katika kutoa mafuzo hayo.
‘’Niseme tu kwamba yote mliyotuelekeza tumeyasikia na kuyaelewa na tunahaidi kuyafanyia kazi lakini pale ambapo tutajihisi tumesahau moja ya mambo tuliyojifuza tutahitaji tena ushirikiano wenu wa kutufundisha ‘’, amesema Mhe.Menasi.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe amewapongeza Viongozi wa Chama wakiongozwa na Mhe.Constantine Morandi na Timu ya Wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Zahara Michuzi kwa utendaji kazi wao.
‘’Vile ambavyo tumekuja sio sawa na sasa tunavyoondoka kwakweli mumeweza kukata kiu zetu, pia mumetujengea uelewa wa utekelezaji wa miradi ya Cooperate Social Responsibilities (uwajibikaji wa kampuni kwa jamii inayozunguka mradi) kitu ambacho tulikua hatuna uelewa nacho hivyo haya mliyotufunza tunaenda kuyatendea kazi’’, amesisitiza Ndugu Neema.
Katika ziara hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Songea wametembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Halmashauri ya Mji Geita kupitia Miradi ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii inayozunguka Mradi ikiwemo Mradi wa Soko la Dhahabu, uwanja wa mpira, Shule ya msingi Bombambili na Machinjio ya kisasa.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Septemba 21, 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa