HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea imetekeleza afua ya lishe ya robo ya nne kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, wamama wajawazito na vijana walio katika umri balehe.
Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Kamando Mgema katika kikao cha utekelezaji wa tathmini ya mkataba wa lishe kilichoudhuriwa na viongozi na wataalamu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Lundusi Peramiho.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022 Milioni 36 zilitengwa na zimetumika katika kutekeleza afua mkataba wa lishe.
Pia amesema fedha hizo zilitengwa kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri na nyingine kutoka katika mfuko wa pamoja wa afya.
‘’Nawapongeza viongozi wote kuanzia ngazi ya kata na kijiji katika usimamiaji na kutoaji wa taarifa za maeneo yenu hivyo kumekua na mwelekeo chanya wa utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe’’, amesema DC Mgema.
Kwaupande wake Afisa Lishe Joyce Kamanga amesema katika robo hii ya nne ya mwisho kuna baadhi ya kata ambazo walibaini watoto saba wenye wenye utapiamlo ambao watoto watatu wanaendelea na matibabu na wanne wamepona.
Aidha amesema zoezi hili limefanikiwa kutokana na uwepo wa uwajibikaji wa pamoja wa viongozi kwa kutoa fedha za utekelezaji wa afua za lishe kwenye ngazi ya Wilaya.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Septemba 09 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa