Katika kuadhimisha Wiki ya unywaji wa Kahawa Duniani, Uongozi wa Kampuni ya Aviv umeadhimisha pamoja na Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kwa kushiriki matukio mbalimbalo ya kijamii
Hafla hiyo iliandaliwa ili kuenzi mchango mkubwa wa zao la kahawa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, huku ikilenga pia kuhamasisha mshikamano na afya kwa njia ya michezo.
Tukio hilo lilihudhuriwa na wakulima, maafisa ugani pamoja na viongozi wa halmashauri, wote kwa pamoja wakionyesha ushirikiano wa dhati.

Michezo kama mpira wa Miguu ulifanyika kwa ari na mshikamano mkubwa kati ya timu ya Shamba la Kahawa na halmashauri.
Sherehe hizo pia zilipambwa na unywaji wa kahawa, ambako washiriki walipata fursa ya kujifunza kuhusu mbinu bora za uzalishaji na usindikaji wa kahawa.

Maadhimisho haya yameacha alama ya mshikamano, maarifa na hamasa mpya kwa jamii ya wakulima wa kahawa, huku yakisisitiza umuhimu wa kulinda na kuendeleza zao hili muhimu.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa