MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya Songea Mheshimiwa Menace Komba ameendesha mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani uliodhuriwa na Viongozi wa chama cha siasa na wataalamu.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Lundusi Peramiho tarehe 02 Septemba 2022.
Lengo la mkutano huo ni kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, kuunda kamati za kudumu pamoja na kupokea taarifa ya mwaka.
Mwenyekiti Menace amempongeza Simoni Boniface Kapinga kwa kupata kura zote za ndio na kumtangaza kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea pia amewapongeza Madiwani walioteuliwa katika kamati za kudumu.
‘’Pamoja na uteuzi huu wa kamati tunategemea kila aliyechaguliwa kutoa ushirikiano mkubwa katika kamati aliyoteuliwa hili Halmashauri yetu iweze kusonga mbele Zaidi kwa maendeleo’’ amesisitiza Mheshimiwa Menace.
Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amewapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa kushika nafasi ya tano Kitaifa kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.
Aidha amesema kila mtu akiwa kielelezo kwa kuwa msaada katika kukusanya mapato tutafika mbali sana.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
05 Septemba 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa