Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, ulitembelea na kukagua Soko la mazao la Kimkakati lililopo kijjiji cha Matomondo kata ya mbingamhalule Halmashauri ya Wilaya ya Songea, na kujiridhisha na namna linavyoenda, hivyo kukubaliana kuwa soko hilo kuanza kufanya biashara mwezi mei 2024
Mradi wa Ujenzi wa Soko na Ghala katika kijiji cha Matomondo uliingiziwa kiasi cha shilingi 198,795,000.00/= kutoka Serikali kuu na baadae iliongezewa kiasi cha shilingi TZS. 20,000,000.00/= kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi kutoka maato ya ndani ya Halmashauri.
Soko hilo lenye jumla ya majengo manne ikiwemo choo, Ghala pamoja na shedi mbili, linategemea kuanza biashara mwanzoni mwa mwezi wa Tano kama kila kitu kitaenda vizuri.
“Kwanza kabisa kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea, tunapenda kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuwezesha fedha ambazo zimetumika kujenga soko hili la Kimkakati hapa Matomondo.
Ruvuma hasa wilaya ya Songea, inawakulima wengi wa mazao ya chakula, hivyo kwa kuweka soko hili litasaidia kukuza uchumi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, lakini pia itawasaidia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuuza mazao yao kiurahisi.” Alisema Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambaye ndiye aliyeongoza Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa