SIMAMIENI UJENZI WA BARABARA.
Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi OfisI ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Ajira Vijana na watu wenye ulemavu Mh Jenista Mhagama amewaagiza Wakala wa barabara Mijini na vijijini kuhakikisha wakandarasi walio pewa mkataba wa kujenga barabara wanakamilisha kwa wakati
Mh Jenista ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea hivi karibuni.
Mh Jenista amewaagiza wakala wa barabara Mijini na Vijijini wahakikishe wa kandarasi wliopewa dhamana ya kujenga barabara wanakamilisha kwa wakati kulingana na mikataba yao na barabara hizo ni Liganga kuelekea Mbolongo hadi Mwimbasi yenye urefu wa kilomita 30 na barabara ya Mgazini hadi Mhepai yenye urefu wa kilomita 7 zote zikiwa na thamani ya shilingi milioni 340.
Amesema barabara ni fursa ya kiuchumi hasa sekta ya kilimo na mawisiliano ya usafiri na usafirishaji inakuza uchumi katika jamii na inaingiza mapato Serikalini kupita ushuru,na kodi mbalimbali zinatozwa.
Naye kaimu meneja wa wakala wa barabara Mijini na Vijijini wa Halmashauri ya Wilaya Songea Bw Simoni Binamu amesema hawata sita kuwachukulia hatua za kisheria wakandarasi wiliopewa kazi ya kujenga barabara endapo wataenda kinyume na mkata wao wa kazi.
Amesema hatua ambazo wanaweza kuchukuliwa ni pamoja na kutozwa faini ya asilimia 10 ya malipo yao na kuvunja mkataba wa kazi,na mkataba huo umeanza mwezi machi 26 na kuishia julai 26 2018.
JACQUELEN CLAVERY- TEHEMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa