SHIRIKA lisilo la Serikali (ROA) limetambulisha Mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya Rasilimali za Umma(PETS) kwa Viongozi wa Chama na Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Utambulisho huo umefanyika leo Septemba 30, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Lundusi- Peramiho.
Akizungumza katika utambulisho huo Mratibu wa Mradi wa ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma Dadiely Chanachayo amesema ROA imedhamiria kuboresha mahitaji ya msingi kwa binadamu ikiwemo afya, Utawala bora na haki za watoto.
‘’Kama tunavyojua afya ni kitu ambacho binadamu yoyote bila afya nzuri hawezi kuishi kwa amani hivyo lengo la taasisi hii ni kuangalia na kufatilia kwa makini kwenye swala zima la afya kwa kuboresha huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya’’, amesema Chanachayo.
Hata hivyo amesema ifikapo wiki ijayo wamedhamiria kutembelea na kutekeleza Miradi katika sekta ya afya kwa kata tatu zilizopo Songea vijijini ambazo ni Matimira, Litisha na Magagura.
Amesema wanaenda kufanya mikutano kwenye ngazi ya vijiji ili kwenda kuchagua wajumbe wa kamati ya PETS ambao wana uwezo mzuri wa kusoma, kujieleza na kujiamini.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menasi Komba amewapongeza kwa jitihada wanazofanya katika kuboresha huduma za afya.
Pia amewataka wataalamu hao kuwajengea wananchi uelewa kushirikisha katika suala zima la ujenzi kwani litaongeza usimamizi mzuri na ulinzi wa kutosha katika rasilimali hizo.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Septemba 30, 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa