SHIRIKA la PADI kuanza kutoa mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto wakiume
Shirika lisilokuwa la kiserika la kuhudumia watu wasiojiweza na wenye Ulemavu ( PADI) linatarajia kuanza kutoa mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kiume wenye umri wa miaka tisa hadi 14 katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Meneja mradi Gifti Kilasi amesema kupitia mradi wa USAID KIZAZI KIPYA unaosimamiwa na PADI utaanza kutoa mafunzo kwa watoto hao ili waweze kufahamu madhara ya ukatili wa kijinsia na waanze kupinga ukatili huo katika jamii.
Amesema mafunzo hayo yatasaidia kuandaa Taifa la vijana wakiume wenye maadili mema , kuondoa migogoro, kupambana na kupinga matendo maovu ya ukatili wa kijinsia sambamba na kuongeza upendo na mshikamano katika jamii
“Matendo mengi ya ukatili wa kijinsia yanasababiashwa na wanaume”,amesema Kilasi.
Kilasi amesema wamegeukia kundi hilo kwasababu ni kundi ambalo ni wahanga wa ukatili wa kijinsi,na kundi ambalo lilisahaulika katika kuwapa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ukilinganisha na watoto wa kike.
Afisa Ustawi wa Halmashauri ya Wilaya ya songea Suzana Mkondya amewaasa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwasadikisha watoto wakiume kuwa majasiri ,kwani hali hiyo ni kikwazo kwa watoto wakiume kutambua madhara ya ukatili wa kijinsia na kutoa taarifa pale wanapofanyiwa vitendo hivyo katika jamii.
“Wewe ni mtoto wa kiume kuwajasiri”,amesema Mkondya.
Amesema baada ya mafunzo hayo wanatarajia vitendo vingi vitaripotiwa katika vyombo vya dola na kutolea maamuzi ya kisheria,hata hivyo siku zitakavyo zidi kwenda mbele matendo hayo yatapungua kwa kiasi kikubwa na watoto wataelika na kuanza kutoa elimu kwa vijana wengine.
Ameongeza kwakusema mafunzo hayo yatatolewa kwa nadharia na vitendo kupiti michezo na yatafundishwa na walimu wa shule za msingi katika maeneo husika,pia watoto watapata fursa ya kupima magonjwa endapo watapatikana na matatizo ya kiafya hasa vvu.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Zena Ibrahimu ametoa wito kwa wadau wa mradi huo kusimamia vizuri na kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezaji wa mradi huo ili uweze kutoa matokeo chanya ya kujenga na kulinda maadili mema Yakitanzania.
Mradi huo utaanza kutekelezwa Oktoba mwaka huu tayari wameshasajili watoto 2700 wa shule za Msingi na lengo ni kuwa fikikia watoto 8000 hadi kufikia mwezi Septemba 2021 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Watoto katika zoezi hilo watapatikana kutoka katika Kata ya Parangu,Maposeni,Kilagano,Litapwasi,Mpitimbi,Kizuka,Litisha na kata nyingine ni Magagara,Peramiho na Mbinga mhalule,kwakila kata zimechaguliwa shule tatu mradi wa USAID KIZAZI KIPYA umeanza kutekelezwa mwaka 2017 na utafikia mwisho wake mwezi Septemba 2020
Imeandikwa na Jacquelen Clavery
Afisa habari songea dc
Septemba 10,2020
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa