HALMASHAURI ya Wilaya ya Songea imepokea fedha zaidi ya shilingi milioni 560 kupitia program ya uboreshaji Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe amesema shule hiyo mpya inajengwa Kata ya Kilagano katika shule ya Sekondari Lugagara.
“Kwa niaba ya Viongozi na Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea namshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kuendelea kuleta fedha za kuboresha miundombinu ya elimu na kuondoa changamoto za uchache wa madarasa”, amesema Ndugu Neema.
Aidha, amesema kwa kushirikiana na wataalam atahakikisha mradi unasimamiwa kwa umakini ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa