Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenelali Balozi WILBERT IBUGE amesema serikali itaendelea kusimamia na kuimarisha mfumo wa stakabadhi ghalani kwa mazao ya ufuta,soya na mbaazi ambayo yanatakiwa kuuzwa kwa mfumo huo kwa msimu wa kilimo wa 2021/2022.
Balozi Ibuge ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma .
Balozi Ibuge ameyataja baadhi ya mafanikio ya mfumo wa stakabadhi ghalani kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 ni pamoja na kuwepo kwa bei ya makubaliano baina ya wakulima na Makampuni yanayonunua mazao hayo,wakulima kulipwa fedha zao kwa wakati na Serikali kukusanya maduhuri yake kupitia ushuru na tozo.
Amesema usimaizi na ufuatiliaji wa mfumo huo umesaidia pia kuimarisha uchumi wa kipato kwa wananchi kwakuwa mazao hayo yamekuwa yakiwapa faida wakulima,kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/2021 zao la ufuta limewaingizia Shilingi Bilioni 17.221,852,087 zao la soya na mbaazi ziliingiza Bilioni 9.3
Ameongeza kwa kusema katika kuendeleza Sekta ya kilimo Mkoa umeanda shughuli za kilimo cha pamoja na kilimo cha mkataba ambacho kitaongeza tija na uzalisha kwa mkulima kwa mazao ya ufuta,soya na alizeti ambapo jumla ya ekari 48,343 zimetengwa kwa Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma.
Kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa hufanyika kila mwaka kikiwa na lengo la kujadili utekelezaji wa chngamoto katika sekta mabalimbali zikiwemo Afya,Maji,Mamlaka ya Mapato Tanzania ,Elimu nyingine ni Umeme na Ardhi.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa