Mratibu wa TASAF kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri tayari wameanza kusimamia uibuaji wa miradi ya kutoa ajira za muda (PWP) kwa walengwa wa mpango wa TASAF III. Uibuaji wa miradi hiyo unazingatia vimbaumbele vilivyowekwa na wanakijiji katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya kijiji husika.
Wanaviji walio katika mradi wa Tasaf III wamepatiwa fursa ya kuibua miradi hiyo ili iweze kuwasaidia walegwa na jamii nzima ya kijiji husika.
Aidha katika msimu uiopita Tasaf III ilitekeleza miradi mbalimbali iiwa pamoja na uboreshwaji wa visima vya asili, ujenzi wa vivuko vya kwenda mashambani na upandaji wa miti.
Miradi hiyo imesaidia wananchi kupata maji safi na salama kwa matumizi ya wanavijiji na kuhifadhi mazingira yanayozunguka vyanzo vya maji kwa kupanda miti rafiki ya maji.
Wananchi wamenufaika na ujenzi wa vivuko vya mashambani kwa kurahisha uvukaji kipindi cha masika ambapo mito mingi hufurika na kusabibisha wananchi kushindwa kuvuka kuelekea mashambani. Pia vivuko hivyo vitasaidia msimu wa mavuno wananchi kupitisha mazao yao kwa urahisi.
Mradi wa miti umekuwa ni mradi unaopendwa sana na jamii kutokana na faida zake. Wananchi wamekuwa wakijitahidi kupanda miti ili kuhifadhi mazingira pamoja kujipatia mazo ya miti kama matunda na mbao.
Mratibu wa Tasaf III amewataka walengwa wa mradi wa ajira za muda (PWP) kushiriki katika kazi za muda ili waweze kujipatia kipato cha kujikimu kipindi cha Hali.
Miradi hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa mwanzoni mwa mwezi septemba na kumalizika mwezi Disemba mwaka huu
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa