MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka wananchi mkoani humo kuacha kusafisha mashamba kwa moto kwani uchomaji huo umeleta athari kubwa za kimazingira.
Kanali Thomas ameyasema hayo katika kijiji cha Liparamba wilayani Nyasa wakati alipofanya ziara na kuzungumza na wananchi alisema utaratibu wa kusafisha mashamba kwa kuchoma moto umepitwa na wakati hivyo amewataka viongozi wa vijiji kuunda kamati za utunzaji mazingira
“Utunzaji wa mazingira ni jukumu letu sote, sisi wenyewe ni mashahidi miaka ya nyuma kipindi kama hiki mvua ingekuwa tayari imeshanyesha hii yote ni athari ambayo tunasababisha katika mazingira kwahiyo tuache kuchoma moto mashamba”, amesema Kanali Thomas.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa