Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa maagizo kwa viongozi wa Ushirika na wadau wa kilimo kwenda kuhamasisha wakulima kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao la soya.
Mndeme ametoa maagizo hayo kwenye mkutano wa tathimini ya wadau wa mazao mchanganyiko yanauzwa kwa mfumo wa stakabathi ghalani kilicho fanyika katika manispaa ya Songea hivi karibuni.
“Natoa maelekezo kwa wakulima,vyama vya ushirika,vyama vikuu nya ushirika,wafanyabiashara,kamati zinazosimamia minada na wadau wote wanaoshiriki minada kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ili zoezi la uuzaji na ununuzi wa mazao liweze kufanyika kwa ufanisi na kumnufaisha mkulima wa mkoa wa Ruvuma”,amesema mndeme.
Mndeme amesema zao la soya kwa msimu wa kilimo 2021/ 2022 limekuwa na soko kubwa ukilinganisha na hali halisi ya uzalishaji wake wa tani 7844 hitaji likiwa tani lakimbili.
Ameongeza kwa kusema wadau wa ushirka na kilimo wahakikishe mkulima hadhulumiwi haki yake nawafuatilie na wasimamie utaratibu wa soko la mfumo wa stakabadhi ghalani na kujiepusha na ubadhirifu wa aina yoyote ambao unalenga kumwibia mkulima.
Naye Mrajisi Masidizi wa vyama vya Ushirika wa Mkoa wa Ruvuma Bumi Musuba amesema maandalizi ya soko kwa mazao yanayouzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa msimu wa 2021/2022 ambayo ni ufuta ,soya na mbaazi yataendelea kuuzwa kwa mfumo huo ambao utasimamiwa na Serikali kupitia vyama vikuu vya Ushirika vya SONAMCU LTD na TAMCU LTD.
Musuba amesema mfumo wa stakabadhi ghalani unafaida kwa wananchi kwavile unaongeza pato la mkulima,Halmashauri zinakukusanya ushuru, kutoa ajira za muda kwa wananchi pamoja na ukusanyaji wa kodi kwa kawa upande wa TRA.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mpinduzi wa Mkoa wa Ruvuma Nuru Ngereja amesema katika kuongeza tija kwenye zao la soya ni vema wakulima wakafikishiwa pembejeo kwa wakati sanjari na kuwapa elimu na usimamizi utakao msaidi kuvuna mazao mengi.
Japhari Mapunda ni miongozi vya viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika amesema wanatoa shukrani kwa viongozi wa Serikali na Ushirika kwa kupunguza toza za wakulima toka sh.70 kwa kilo hadi sh.35 jambo ambalo litawasaidia kutatua changamo kwenye vyama vyao.
Mkoa wa Ruvuma unatarajia kukusanya na kuuza tani15,437 za ufuta,tani7844 za soya na tani 2889 za mbaazi.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari Songeadc
13/04/2021.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa