Katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma steven Ndaki ahimiza ukamilishaji wa ujenzi wa miradi sambamba na utoaji wa huduma
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Steven Ndaki amehimiza ukamilishaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Ndaki amesema hayo alipotembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya Songea hivi karibuni.
Ndaki amesema nimeridhishwa na ujenzi wamiradi inavyoendelea kujengwa pia kazi ni nzuri napongeza,dosari ndogo ndogo ambazo zinatakiwa kurekebishwa zirekebishwe.
“Jitihada iongezwe ili miradi ikamilike na ianze kutoa huduma kwa wananchi”,alisema Ndaki.
Ametoa wito kwa wananchi kuanza kupata matibu katika Hosptali ya Wilaya ya Mpitimbi ambayo imeanza kutoa huduma hiyo kuanzia Julai 15 mwaka huu ,badala ya kutembea umbali mrefu na kutumia gharama kwaajili ya kufuata huduma ya matibu katika hospitali ya Mkoa na Peramiho.
Ameongeza kwa kusema katika ujenzi wa miradi ya maendeleo inyotekelezwa ndani ya mkoa kwa njia ya force akaunti swala la uzalendo ni muhumu likapewa kipaumbele kwasababu linalinda maslahi na uaminifu katika ujenzi na utekelezaji wa mradi husika.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw Simon Bulenganija ameshukuru timu ya ukaguzi kwakukagua miradi na kutoa mapendekezo ambayo yanasaidia kuboresha ujenzi wa miradi hiyo.
Bw Bulenganija amesema jitihada za ukamilishaji wa miradi zitaongezwa na miradi itakamilika na kuanza kutoa huduma kama lengo la serikali linavyoelekeza la utoaji huduma kwa wananchi hasa wanyonge.
Jumla ya miradi nane ilikaguliwa ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya cha Matimira na Magagura, Hosptali ya Wilaya iliyopo Mpitimbi,pamoja na miradi mitano ya ujenzi wa vyoo bora (SWASH) vinavyojengwa katika shule za Msingi Mpitimbi, Mkurumusi,Peramiho ,Mapinduzi na Humbaro
Imeandikwa na
JACQUELEN CLAVERY
AFISA HABARI SONGEA DC.
19 /08 / 2020.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa