Serikali kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari Nchini (SEQUIP) imetoa shilingi milioni 600 kujenga shule ya sekondari katika Kijiji cha kizuka Kata ya Kizuka Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Afisa mipango wa Halmashauri hiyo Nyange Athumani amesema fedha hizo zitatolewa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza imetoa shilingi milioni 470 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa mradi huo.
Nyange ameitaja miundombinu ambayo inaanza kujengwa kuwa ni vyumba nane vya madarasa,maabara tatu za sayansi,jengo la utawala,maktaba,chumba cha TEHAMA,vyoo vya wanafunzi matundu 10 kwa wasichana na wavulana miundombinu mingine ni tanki la maji la lita 10,000 na nguzo yake na miundombinu ya kunawa mikono na kuvuna maji.
Nyange amesema fedha za ujenzi wa shule hiyo zimeshaingizwa kwenye akaunti ya shule ya Sekondari Magagura pia taratibu za kuanza ujenzi zimemeshafanyika ikiwa na pamoja na kutambulisha mradi kwa wananchi kupitia mkutano wa hadhara na kuunda kamati zitakazo husika na usimamazi wa mradi.
Ameongeza kwakusema awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za walimuna ununuzi wa vifaa vya chumba cha TEHAMA ambapo serikali itatoa kiasi cha shiringi milioni 130 kwa kukamilisha miradi hiyo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kizuka Mhe.Jakob Nditi amemshukuru Rais wa awamu ya sita Mhe Samia Suluhu Hassani kwa kuwapatia fedha wananchi wa Kata ya Kizuka za ujenzi wa shule ya sekondari ambayo inakwenda kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali umrefu kufuata masomo katika shule sekondari ya Magagura.
Mhe. Nditi amesema wananchi wa Kata hiyo wameshatoa eneo lenye ukubwa wa ekeri 35 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na wapo tayari kushirikiana bega kwa bega na wataalam katika kufanikisha ujenzi wa mradi huo.
Wamesema kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kutasaidi kuongeza ari ya watoto wao kusoma na kutotembea umbali mrefu kufuata masomo katika shule ya sekondari ya Magagura.
Mradi wa SEQUIP unalenga kuongeza fursa ya upatikanaji wa elimu ya Sekondari ,kuweka mazingira salama ya elimu kwa wasichana na kuhakikisha wanafunzi wote wanapata elimu bora ya sekondari.
Kujengwa kwa shule hiyo kunafikisha idadi ya shule 17 za sekondari zinazomilikiwa na Serikali kwa kata zote 16 za Halmashauri hiyo na kuondoa changamoto ya upungufu wa shule za sekondari kwa sasa.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa