NATIONAL MICROFINANCE BANK (NMB) KUENDELEA KUSAIDIA JAMII
WAZIRI Wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Sera Bunge Ajira Vijana Walemavu Mh Jenista Mhagama amepokea Msaada wa Madawati 150 yenye thamani ya Shilingi Milioni 10 Kutoka Bank ya NMB.
Madwati hayo yamekabidhiwa na kaimu meneja wa NMB Bank kanda ya Mtwara Bw Frank Rutakwa katika hafla fupi iliyofanyika katika shule ya msingi Mipeta iliyopo Kata ya Mhukuru wilayani Songea hivi karibuni.
Mh. Jenista Mhagama ameipongeza Bank ya NMB kwa kusaidia jamii kupitia misaada mbalimbali wanayoitowa kwa wananchi kama huduma za Elimu, Afya n.k.
Bank ya NMB imetoa msaada wa madawati 150 yenye thamani ya shilingi milioni kumi, Masada huo umetolewa kufuatia changamoto ya upungufu wa madawati katika shule hiyo.
Bw Rutakwa amesema bank ya NMB nisehemu ya jamii hivyo inawajibu wa kuisaidia jamii katika huduma zakijami.
Shule ya Msingi Mipeta inajumla ya wanafunzi 354 na walimu 6
Imeandaliwa na
Jacquelen Clavery -Habari mawasiliano na Mahusiano kazini.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa