Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Kanali. Ahmed Abbas Ahmed, amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kwa namna wanavyoshirikisha wanacnhi kwenye kutekeleza miradi.
Mkuu wa Mkoa, ameyasema hayo leo wakati akipokea taarifa ya muendelezo wa ujenzi wa Standi ya Kisasa iliyopo kata ya Peramiho kijiji cha Lundusi Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Akisoma taarifa Mratibu wa TASAF, Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi. Hossana Ngunge alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa mnamo mwezi June mwaka 2022, wananchi wa kijiji cha Lundusi kupitia Mkutano halali wa hadhara wa jamii waliibua mradi wa ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya kisasa kupitia mpango wa TASAF na kupeleka maombi ya Fedha TASAF Makao Makuu
“ ambapo baadae kiasi cha Fedha Shilingi Milion Mia nne thalathini na nne, laki sita hamsini na saba elfu mia nane na mbili na senti sitini na nane ( TSH. 434,657,802.68) ziliwekwa kwenye akounti ya Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu wa Stend ya Mabasi
Fedha hizo ni kwa ajii ya ujenzi wa Jengo la Utawala, Maduka 36, Vibanda vya walinzi viwili, vyoo matundu nane (8) pamoja na uzio
" niwapongeze sana kwa usimamizi mzuri wa mradii huu, uliofanywa na viongozi lakini pia wanakamati nimekagua, nimepokea taarifa, tuseme nimefarijika sana kwa utekelezaji wa mradi huu, hasa ushirikishwaji wa wananchi toka hatua za mwanzo nimefurahishwa pia wananchi/ wanakamati wanajua hadi kiasi cha Fedha kilichobaki"
Lakini pia kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Hosana Ngunge alimshukuru Rais wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu hassani kwa kuwaletea fedha za ujenzi wa miundombinu ya Stendi.
Shukrani pia zilitolewa kwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama kwa kujitoa kwake kwa ajili ya wananchi wake.
Pamoja na hayo Mratibu alimshkuru pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya WIlaya ya Songea, Mhe. Menans Komba, kwa ufuatiliaji wa miradi ndani ya Halmashauri ya Songea lakinin pia Diwani kata ya Peramiho kwa ushirikiano anaoutoa katika utekelezaji wa miradi ndani ya Kata ya Peramiho.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa