Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma yapongeza ukarabati wa wa skimu ya umwagiliaji iliyopo Muhukulu wakati wa ziara yake iliyofayika tarehe 9 Octoba 2023 katika Kijiji hicho.
Akizungumza na wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea pamoja na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Komredi Odo Mwisho ameeleza kwamba mradi huo utakapo kamilika utafungua milango mikubwa ya kiuchumi kwani WAKULIMA watafanya kilimo bila kuangalia kama mvua inanyesha au hainyeshi. Ambapo amesema
" Huu ni moja kati ya miradi mikubwa ambayo inapatikana nchini Tanzania ambao ukamikaji wake utafungua fursa nyingi za kiuchumi hususani kwenye kilimo ambapo wakulima watakao utumia mradi huu watalima muda wote bila kuangalia mvua inanyesha au hainyeshi kwasababu maji ni yakutosha hii yote inaonesha ni namna gani Raisi wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anawapenda wakulima wa Mkoa wa Ruvuma ndio maana ametenga fedha nyingi sana ili kukamilisha huu mradi hivyo niwaombe ndugu zangu kutoa ushirikiano kwa Mhe Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo".
"Basi pamoja na mambo mengina napenda kumshukuru Mhe Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwani kuleta maendeleo kama haya ni moja ya utekelezaji wa Chama chetu, pia kipekee napenda kuishukuru Kamati ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma kwa kuendelea kukitangaza vyema Chama cha Mapinduzi kwa kutekeleza ilani ya Chama chetu kwa kusimamia maendeleo ya miradi mbalimbali, pia nimshukuru Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Joakim Mhagama kwa ufuatiliaji mzuri wa maendeleo katika Jimbo lake, pia nakushukuru Mkuu wa Mkoa na timu Yako, Mwenyekiti wa Halmashuri na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Songea na timu Yako ya utendaji pamoja na Baraza la Madiwani kwa pamoja tunasema kidumu Chama cha Mapinduzi kidumu Chama Tawala".
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mhandisi anayesimamia mradi huo amesema "Mwajiri wa mradi huu ni timu ya Taifa ya umwagiliaji kutoka makao makuu Dodoma na Mkandarasi ni Muungano yaani Joint venture General Interpises kwa staff ya Limited kutoka Iringa, na thamani ya Mradi huu ni shilingi 986,267,035.00 na mradi unatarajiwa kukamilika Tarehe 21 Januari 2024".
"Ambapo ujenzi wa mradi huu unahusisha vitu vifuatavyo -; ujenzi wa banio, ujenzi wa mfereji wa maji wenye urefu wa km2 na m200, kujenga vivusha maji na barabara yenye urefu wa km2, mpaka sasa tumefikia 57.7%za ujenzi wa mradi huu na malipo ya awali yamefanyika ambapo Mkandarasi amelipwa shilingi 137,361,960.73 ambayo ni sawa na asilimia 31%ya malipo yote.
Nae Mkandarasi ameahidi kukamilisha ndani ya wakati ambapo amesema "Kama mnavyoona tulikuwa na zoezi la uchevushaji wa maji na limekamilika, pia ujenzi wa banio nalo limeisha barabara nayo imekamilika kwa kiasi chake ambapo kw sasa Bado tu kuweka makaravati, kwa ujumla kazi kubwa iliyobaki kwa sasa ni kukamilisha mifereji ya maji na ninaamini mpaka kufikia hiyo Januari nitakuwa nimekamilisha huu mradi"
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa