Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto Mhe. Mwanaidi Hamis Ali amewaagiza Maafisa wa maendeleo ya jamii kusimami stahiki za wanawake zinazojuisha umiliki wa mali ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mhe. Ali ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kutembelea kikundi cha wajasiriamali wadogo cha Ukombozi kilichopo Kijiji cha Peramiho Kata ya Peramiho ,Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma hivi karibuni.
Mhe.Ali amesema katika dhana ya wanawake kujikwamua kiuchumi bado kunachangamoto ambazo zimekuwa zikikwamisha jitihada za wanawake kushindwa kumiliki mali ikiwemo ardhi na nyumba kutokana na mitizamo hasi ya kwenye jamii.
Mhe Ali amevitaja baadhi ya vitendo ambavyo vimekuwa vikukwamisha jitihada hizo kuwa ni ukatili wa kijinsia,dhuluma, udhalilishaji,ubaguzi na mila potofu ambazo zinamkandamiza mwanamke katika kumiliki mali na kuendelea kuonekana kuwa dhaifu kwenye jamii.
Ameongeza kwakusema uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi utasaidi kuleta usawa na ustawi wa jamii lakini bado kundi kubwa la wanawake wanaonekana kubaki nyuma na kuonekana kuwa dhaifu katika kujikwamua kiuchumi.
“Nawaagiza Maafisa maendeleo ya jamii kuongeza kasi ya kuhamasiha jamii kujiunga na vikundi vya kiuchumi na kutoa elimu ya ujasiriamali ili Serikali iweze kuwapa mikopo yenye masharti nafuu kupitia mifuko ya uwezeshaji ya wananchi kiuchumi”,amesisitiza Mhe Ali.
Amewahimaza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuendelea kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya kuwawezesha wanawake kuimarisha vikundi vyao vya kiuchumi kwasababu swala hilo lipo kisheria.
Amewataka wanawake kuzingatia taratibu za kukopa na kurejesha mikopo wanayo kopa ili kutoa fursa kwa wengine kuweza kukopa na kunufaika na mikopo hiyo.
Amewarai wazazi na walezi kuendelea kutoa elimu ya malezi kwa watoto wao kitendo ambacho kitasaidia kujenga uelewa kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia na kulinda maadili katika jamii,pamoja na wanawake kuachanana tabia ya kukumbatia matatizo ya ukatili wa kijinsia badala yake wayafikishe kwenye vyombo vya kisheria ili haki iweze kutendeka.
Kwaupande wao wanawake hao wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo malighafi wazotumia kutengenezea bidhaa zao kuwa bei ghari,uhaba wa masoko na mikopo ya asilimia 10 iliyotengwa na Serikali kuwa ni ndogo.
Naye Kaimu Afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya songea Zawadi Nyoni amesema kwa kipindi cha mwaka wa fedha cha 2019 hadi 2021 Halmashauri imefanikiwa kutoa mikopo kwa vikundi 22 wenye thamani ya Tsh milioni 82.
Halmashauri ya Wilaya ya songea inazaidi ya vikundi 100 vilivyosajiliw vikijumuisha wanawake,Vijana na Walemavu.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea Dc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa