Mwenyeki wa Kamati ya Siasa wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mhe.Nelly Duwe amewa amwagiza Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Pololet Mgema kuwachukulia hatua mafundi viongozi wanaokwamisha utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Mhe.Duwe ametowa maagizo baada ya Kamati ya Siasa ya Wilaya kufanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo hivi karibuni.
Mhe.Duwe ametoa maagizo hayo kufuatia baadhi ya mafundi viongozi kwenda kinyume na mikataba waliopewa ya kujenga miradi ya maendeleo jambo ambalo linakwamisha jitihada Serikali za kuwafikishia huduma wananchi.
Amesema dhamira ya Serikali ni kuona miradi inayojengwa inakamilika kwa wakati na inatoa fursa na huduma iliyokusudiwa kwa wananchi hivyo mafundi viongozi waliopewa dhamana ya kujenga na kukamilisha miradi ambao wanakiuka utaratibu hawakubariki.
Kwaupande mwingine amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Neema Maghembe kuakikisha anafuatilia na kusimamia miradi yote inayotakiwa kukamilishwa inakamilika na inatoahuduma kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe Menasi Komba amehaidi kufuatilia na kusimamia fedha za mapato ya ndani zinatengwa kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi inayotakiwa ikamilishwe.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Matimira Kijiji cha Matimira wametoa pongenzi za dhati kwa Serikali kwakuwajengea kituo cha Afya ambacho kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 400 kukikamilisha nao waanze kupata huduma ya matibabu na kuepukana na adha ya kufuata huduma hizo umbali mrefu ambapo ujezi wa kituo hiko ulianza mwezi Mei 2020.
Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Songea imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Vituo vya Afya na Zahanati ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari na kupokea taarifa ya ujenzi wa mradi wa shule ya sekondari ya Jenista Mhagama inayojegwa Kata ya Parangu Kijiji cha Parangu.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa