Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Mhe. Komredi Odo Mwisho apongeza maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mpitimbi A Kata ya Mpitimbi baada ya kutembelea mradi huo mnamo Tarehe 9 Octoba 2023 wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma ikipita kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Alitoa pongezi hizo amewaomba wasimamizi wa mradi hou kuharakisha ujenzi wa Zahanati hiyo ili kupungunza umbali kwa wananchi kufuata huduma za afya kwenye Kijiji jirani kwani kukamilika kwa mradi huo utawapunguzia adha ya usumbufu wa gharama na umbali kwa wananchi wa Kijiji cha Mpitimbi A. Ambapo amesema
"Tunatambua juhududi kubwa zilizofanywa na wananchi wa Kijiji cha Mpitimbi A kwenye kuanzisha mradi huu nami nasema mnastahili pongezi kubwa kwa kujitoa kwenu hivyo serikali ilitambua jitihada zenu na kuamua kuwashika Mkono kwa kutoa Milioni 50 ili kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa asilimia miamoja(100%) Rai yangu kwenu ni kuhakikisha fedha hizi zinakamisha mradi huu kwa asilimia zote na wananchi waweze kifurahia huduma bora zitokanazo na Serikali kuu kupitia kwa Raisi wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan "
"Mwisho napenda kuishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan Raisi wetu kwa kuona umuhimu wa wananchi wake na kuamua kutoa fungu la fedha kuhakikisha Zahanati hii inakamilika, pia nakushukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa usimamizi mzuri wa miadi ya hapa Mkoani kwako ikiwemo huu wa Zahanati, pia Shukrani zimfikie Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Joakim Mhagama kwa kujitoa kwake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea pamoja na timu yake ya utendaji pamoja na Madiwani wote katika kuhakikisha ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa".
Mradi huu wa ujenzi ulianza rasmi mwaka 2017 kupitia nguvu za wananchi na viongozi kwa kuliona hilo waliwashika Mkono wananchi kwa nyakati tofautitofauti ili kuhakikisha mradi huu unakamilika akiwemo Jenista Joakim Mhagama Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye alichangia milioni tatu, pia Mwenyekiti wa Halmashuri pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea walichangia milioni mbili na lakitano na mwisho Serikali kuu imechangia milioni hamsini ili kukamilisha Zahanati hiyo
Nao wananchi wameishukuru Serikali kwa kuwajali kwani wanasema wanapata taaba ya umbali mrefu kufuata huduma za afya lakini mradi huu utakapo kamilika utawarahisishia sana kwenye suala la huduma za afya hivyo wamesema wanaimani na Serikali yao na wameahidi kutoa ushirikiano.
Mradi huu unatarajiwa kukamilika Tarehe 20 Octoba 2023 na kukamilika kwa mradi huu utapunguza adha ya usafiri kwa wagonjwa kwenda Kijiji cha jirani kufuata huduma za afya.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa