MWENYEKITI wa UWT Taifa Ndugu Mary Pius Chatanda ametembelea na kukagua ujenzi wa madarasa na mabweni katika shule ya Sekondari Jenista Mhagama.
Ndugu Mary Chatanda ameridhishwa na mradi huo na amewataka wanafunzi wasome kwa bidii ili wafaulu kwani Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu.
Aidha, amewasisitiza wazazi kupeleka watoto shule na kuacha tabia ya kuwaozesha watoto mapema.
" Watoto wanapopata nafasi ya kuendelea na masomo wapelekeni shule na hata wanapofeli Serikali imejenga vyuo vya ufundi na inaendelea kujenga hivyo hakikisheni mnawapeleka watoto katika vyuo hivyo", amesisitiza Ndugu Chatanda.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa