MWENGE wa Uhuru umetembelea na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa vijana wa uselemala uliopo katika kata ya Parangu ambao unajihusisha na utengenezaji wa bidhaa za mbao kama madawati, meza na milango, mradi umegharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 38,580,000 na Halmashauri ilitoa mkopo kwa vijana hao fedha kiasi cha shilingi milioni 8 kwaajili ya kununua vifaa.
Akizungumza Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameupongeza uongozi wa Halmashauri kwa kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana ambapo wamesaidia kuongeza ajira kwa vijana.
Aidha, amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii na waendelee kutengeneza bidhaa zenye ubora na viwango vya juu ili waweze kuaminiwa Zaidi na kupewa kazi nyingi ambazo zitawasaidia kupata fedha.
Pia Ndugu Kaim amewataka vijana hao kurejesha mikopo kwa wakati ili mikopo hiyo iweze kukopeshwa kwa wahitaji wengine.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa